BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, April 16, 2012

HAPPY BIRTHDAY LULU


HAPPY BIRTHDAY LULU Leo ni siku aliyozaliwa lulu lakini UTATA wa umri wa Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi inayomhusisha na kifo cha Steven Charles Kanumba ‘The Great’ unazidi kugubika katika ishu hiyo baada ya baba yake mzazi, Michael Edward Kimemeta kuibuka na kutofautiana na watu wengine akiwemo mama ...mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila hivyo kushindwa kung’amua nani muongo na nani mkweli. Uchunguzi umebaini kuwa katika ishu hiyo, kuna mambo mengi yanayosemwa ya uongo na mengine ya ukweli. BABA LULU Mwishoni mwa wiki iliyopita, baba huyo wa Lulu anayeishi Moshi mkoani Kilimanjaro ambaye hakuwahi kusikika kwenye vyombovya habari, alijitokeza kwa mara ya kwanza na kudai kuwa binti yake ana umri wa miaka 16. Baba Lulu alikaririwa: “Mwanangu alizaliwa mwaka 1995, atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili , mwaka huu (leo). Kwa sasa ana umri wa miaka 16.” LULU Kabla ya Kimemeta kugusia hoja hiyo alipokuwa akiwataka Watanzania kutomhukumu bintiye na kuacha haki itendeke, tayari Lulualishaiomba mahakama kurekebisha umri wake kuwa siyo miaka 18 kama ilivyokuwa ikielezwa bali ni 17. “Mheshimiwa hakimu, naomba kurekebisha umri wangu, nina miaka 17 na siyo 18,” Lulu aliiambiaMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipofikishwa mahakamani hapo Aprili 11, mwaka huu. MAMA LULU Kwa upande wake, mama Lulu alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyemzaa Lulu hivyo anajua vyema umri wa bintiye. “Mimi ndiye niliyemzaa Lulu, ana miaka 17,” alisema bila kutaja tarehe aliyozaliwa mwanaye kama alivyofanya baba. HALIMA MDEE Naye Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Halima Mdee alipokwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kumuona Lulu, alidai kuwa aliona cheti cha kuzaliwa cha Lulu kikiwa kinaonesha ana umri wa miaka 17. “Niliona cheti cha kuzaliwa, Lulu ana miaka 17,” ....yoyte kwa yote happybirthdy lulu

No comments:

Post a Comment