BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, April 16, 2012

ALIKIBA AKANUSHA KUHUSIKA NA KUMTOROSHA LULU


Kutokana rumors zilizoenea kitaani na kwenye baadhi ya Vyombo vya habari kuwa Eti msanii Ali Kiba amehojiwa na Polisi baada ya Kushukiwa kuwa eti ni yeye ndiye aliye enda kumtorosha Mwanadada Lulu Nyumbani kwa Kanumba (Siku ile ambayo inadaiwa kuwa Lulu eti alisababisha Kifo cha Steven Kanumba kwa kumskuma na Mwigizaji huyo kujigonga Kisogoni na Kufa papo hapo)
Then baada ya tukio hilo Lulu si alipotea nyumbani kwa Kanumba, basi ndo rumorz zikaenea Ali Kiba ndie aliyemfata na Gari Lulu maeneo ya Sinza vatican na kufanikiwa kuondoka nae eneo la tukio.
Sasa Ali Kiba anasema siku hiyo ya Tukio yeye alikua ufukweni Coco Beach anakula bata, ndo akaskia watu wanaongea kwamba Kanumba kafaa, ndipo yeye akaamua kumvutia wire Lulu na kumuuliza ukweli wa taarifa hizo, lakini Lulu alimjibu sio kweli ila Steven Kanumba ana umwa, basi baada ya Muda akapata simu kutoka kwa Mama mtoto wake flani hivi anayeishi maeneo ya Sinza, akamwambia Kanumba amekufa na mwili wake ameuona ukiingizwa Mochwari.
Kuhusu ishu ya kutokuwepo Dar asubuhi ya siku hiyo Ali Kiba amejibu kuwa Alfajiri ya siku hiyo alisafiri kikazi na kuelekea Malindi Mombasa/Kenya  na taarifa kuwa aliwakimbia polisi si kweli.

No comments:

Post a Comment