MSANII gwiji wa filamu Ester Flavian Mushi, ameweka bayana kuwa tasnia ya filamu nchini haiwezi kufikia kiwango cha kimataifa kutokana na uzembe unaofanywa na wakuu wa kazi hizo.
Flavian (22) ambaye mwaka 2009 alishiriki masuala ya urembo katika ngazi ya kitongoji mjini Tanga na kushika nafasi ya pili na baadaye Miss Dar Indian ocean, alisema viongozi wa filamu wanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya filamu na kwamba wanaangalia sura badala ya kipaji.
“Filamu ya Tanzania inauwezo mkubwa wa kukua lakini kutokana na tatizo la kutokupeana nafasi kwa wasanii wenye vipaji haiwezi kufikia ngazi ya kimataifa,” anasema.
Flavian anasema, baadhi ya wazalishaji (Producer) na wakurugenzi hawaangalii vipaji vya wasanii badala yake wanaangalia uzuri wa mtu hata kama hana kipaji.
“Hili ni tatizo kubwa kwa kuwa hawaangalii kazi hiyo itapeleka ujumbe gani kwa jamii bali yeye anaangalia ninamna gani atauza kazi yake. Maadili yanapaswa kuzingatiwa katika kazi,” anasema.
Kwa mujibu wa Flavian, alianza kushiriki filamu mwaka 2008 ambapo alianza na filamu ya is too late, Fack pregnant, Zawadi ya oparetion, Miss Zinduna, No way Out, Ant Suzi, Big Brother na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment