BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, August 28, 2011

MAMTEI AMEJIPANGA VIZURI MWAKA HUU...



MSANII nguli wa Filamu nchini Cesilia Sengerema (Mamtei), ametamba kuwa mwaka 2011ni mwaka wake na anatarajia kufanya vizuri zaidi kwa kuwa amejipanga kikamilifu.
Hata hivyo Mamtei anasema sanaa kwake ni kazi kwa kuwa anaitegemea kwa asilimi 90 katika maisha yake.
Mamtei ambaye amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kushiriki tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, iliyoandaliwa na Chuzi entertainment, anasema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kujipanga vizuri ili aweze kumudu mazingira ya kazi zake.


Mamtei alijizolea sifa lukuki na kujikusanyia mashabiki wengi kutokana na umahiri wake katika kuigiza, jambo lililowafanya wapenzi wengi wa filamu kuvutiwa sana na vipande alivokuwa akiigiza.
“Kuonekana katika runinga bila mpango haina maana yoyote, ndio maana niliamua kuwa kimya ili nijipange, nahakikisha 2011 nitafanya kitu cha tofauti,”anasema.
Alisema ili kuonyesha ukimya wake kuwa uliku na jambo tayari Filamu yake ya Golden night ambayo ni zawadi ya mwaka mpya imeanza kusambazwa na kampuni ya steps entertainment.
Filamu hiyo ambayo kwa mujibu wa Mamtei alisema itakuwa tofauti na filamu nyingine zilizoingia sokoni hivi karibuni, kwa kuwa imewashirikisha wasanii wakongwe kama Monalisa na Natasha.
Monalisa ambaye ametamba katika filamu nyingi na pia aliyetunukiwa tuzo ya msanii bora wa kike katika tamasha la filamu Zanzibar (ZIFF) lililofanyika mwaka jana. Atashirikiana na mama yake ambaye naye pia ni mkongwe wa filamu (Natasha)
Alifafanua kuwa muunganiko huo ndio utakaoifanya filamu hiyo kuwa tishio kwani hakuna asiyejua kazi inayofanywa na wasanii hao wakongwe, ambao wamejizolea sifa ya kushirikishwa katika filamu nyingi na wasanii wenzao.


Aidha aliongeza kuwa, ili kuwapa raha wapenzi wake ambao hawajamwona kwenye uwanja wa filamu kwa kipindi kirefu, Aprili 2011 ataanza kurekodi filamu yake mpya ambayo alisema bado hajaipatia jina. 

No comments:

Post a Comment